Posts

2. Twamsifu Mungu

1. Twamsifu Mungu kwa Mwana wa Pendo, Aliyetufia na kupaa juu.  Aleluya! Usifiwe; Aleluya! Amin.  Aleluya! Usifiwe, utubariki. 2. Twamsifu Mungu kwa Roho Mtukufu, Ametufunulia Mwokozi wetu. 3. Twamsifu Mwana, aliyetufia, Aliyetwaa dhambi akazifuta. 4. Twamsifu Mungu wa neema yote, Ametukomboa akatuongoza. 5. Tuamshe tena, tujazena pendo, Na moyoni uwashe moto wa Roho.

1. Mwokozi Umeokoa

1. Mwokozi umeokoa, Nimekuwa wako wewe. Damu imenisafisha; Sifa kwa mwana Kondoo.  Utukufu, Halleluya!  Sifa kwa Mwana Kondoo!  Damu imenisafisha,  Utukufu kwa Yesu! 2. Nilijitahidi sana Ila sikupata raha; Bali kwa kumtegemea Nilipata Baraka. 3. Daima namwegemea Damu ikifanya kazi, Nikioga kwa chemichemi Itokayo Mwokozi. 4. Sasa nimewekwa wakfu; Nitaishi kwako wewe: Fahari nashuhudia Ya wokovu wa bure. 5. Nasimama kwake Yesu, Ameponya roho yangu; Ameniondoa dhambi, Anifanye mzima. 6. Nilikuwa kifungoni, Niliteswa na dhambi, Nilifungwa minyororo Yesu akanifungua. 7. Sifa, ameninunua! Sifa, nguvu za wokovu! Sifa, Bwana huhifadhi! Sifa zake milele.

3. Hata ndimi elfu

1. Hata ndimi elfu elfu, Hazitoshi kweli Bwana Yesu kumsifu, Kwa zake fadhili. 2. Yesu, jina liwezalo Kufukuza hofu; Lanifurahisha hilo, Lanipa wokovu. 3. Jina hilo ni uzima; Ni afya amani; Laleta habari njema; Twalipiwa deni. 4. Yesu huvunja mapingu Ya dhambi moyoni; Msamaha, tena nguvu, Twapata rohoni. 5. Kwa sauti yake vile Wafu hufufuka Wakafurahi milele, Pasipo mashaka. 6. Ewe Yesu wangu Bwana, Uwezo nipewe, Kuhubiri kote sana, Wote wakujue.

5. Jina Lake Yesu Tamu

1. Jina lake Yesu tamu; Tukilisikia Hutupoza, tena hamu Hutuondolea. 2. Roho iliyoumia Kwalo hutibika, Chakula, njaani pia; Raha, tukichoka. 3. Jina hili ni msingi, Ngao, ngome, mwamba, Kwa hili napata wingi, Kwangu ni akiba. 4. Yesu, Mchunga, Rafiki Mwalimu, Kuhani, Mwanzo, Mwisho, Njia, Haki, Uzima kifoni. 5. Moyo wangu hauwezi, Kukusifu kweli, Ila sifa zangu hizi, Bwana zikubali. 6. Na utakaponiita, Kuja kwako Bwana, Huko kwako sitaacha Kukusifu sana.

4. Jina La Yesu Salamu

1. Jina la Yesu, Salamu! Lisujudieni, Ninyi Mbinguni, hukumu Na enzi mpeni. 2. Enzi na apewe kwetu, Watetea dini; Mkuzeni Bwana wenu, Na enzi mpeni. 3. Enyi mbegu ya rehema, Nanyi msifuni; Mmeponywa kwa neema, Na enzi mpeni. 4. Wenye dhambi kumbukeni Ya msalabani, Kwa furaha msifuni, Na enzi mpeni. 5. Kila mtu duniani Msujudieni, Kote-kote msifuni, Na enzi mpeni. 6. Sisi na wao pamoja Tu mumo sifani, Milele sifa ni moja, Ni “Enzi mpeni.”

7. Ni Tabibu Wa Karibu

1. Taji mvikeni, Taji nyingi tena, Kondoo mwake kitini, Bwana wa mabwana; Name tamsifu Alikufa kwangu, Ni mfalme mtukufu, Mkuu wa Mbingu. 2. Taji mvikeni Mwana wa bikira; Anazovaa kichwani Aliteka nyara; Shiloh wa wanabii, Mchunga wa watu, Shina na tanzu vya Yese, Wa Bethirehemu. 3. Taji mvikeni Bwana wa mapenzi; Jeraha zake ni shani Ni vito vya enzi, Mbinguni hakuna Hata malaika Awezaye kuziona Pasipo kushangaa.

6. Baba Mwana Roho

1. Baba, Mwana, Roho, Mungu mwenye enzi, Kila tukiamka tunakuabudu Baba, Mwana, Roho, Mungu wa mapenzi, Ewe Utatu, tunakusifu. 2. Baba, Mwana, Roho, wakuaminio Wanakutolea shukrani zao Wanakusujudia malaika nao: Wewe u mwanzo, nawe u mwisho. 3. Baba, Mwana, Roho, sisi tu gizani, Utukufu wako hatuoni kosa; U Mtakatifu, nawe u mapenzi, U peke yako, mwenzio huna. 4. Baba, Mwana, Roho, Mungu mwenye enzi, Ulivyoviumba vyote vyakusifu: Baba, Mwana, Roho, Mungu wa mapenzi Ewe Utatu, tunakusifu.