4. Jina La Yesu Salamu
1. Jina la Yesu, Salamu!
Lisujudieni,
Ninyi Mbinguni, hukumu
Na enzi mpeni.
2. Enzi na apewe kwetu,
Watetea dini;
Mkuzeni Bwana wenu,
Na enzi mpeni.
3. Enyi mbegu ya rehema,
Nanyi msifuni;
Mmeponywa kwa neema,
Na enzi mpeni.
4. Wenye dhambi kumbukeni
Ya msalabani,
Kwa furaha msifuni,
Na enzi mpeni.
5. Kila mtu duniani
Msujudieni,
Kote-kote msifuni,
Na enzi mpeni.
6. Sisi na wao pamoja
Tu mumo sifani,
Milele sifa ni moja,
Ni “Enzi mpeni.”
Comments
Post a Comment