6. Baba Mwana Roho


1. Baba, Mwana, Roho,
Mungu mwenye enzi,
Kila tukiamka tunakuabudu
Baba, Mwana,
Roho, Mungu wa mapenzi,
Ewe Utatu, tunakusifu.

2. Baba, Mwana, Roho, wakuaminio
Wanakutolea shukrani zao
Wanakusujudia malaika nao:
Wewe u mwanzo, nawe u mwisho.

3. Baba, Mwana, Roho, sisi tu gizani,
Utukufu wako hatuoni kosa;
U Mtakatifu, nawe u mapenzi,
U peke yako, mwenzio huna.

4. Baba, Mwana, Roho,
Mungu mwenye enzi,
Ulivyoviumba vyote vyakusifu:
Baba, Mwana, Roho,
Mungu wa mapenzi
Ewe Utatu, tunakusifu.

Comments

Popular posts from this blog

2. Twamsifu Mungu

26. Yesu Unipendaye