9. Yesu Kwetu ni Rafiki
1. Yesu kwetu ni rafiki,
Hwamiwa haja pia;
Tukiomba kwa Babaye
Maombi asikia;
Lakini twajikosesha,
Twajitweka vibaya;
Kwamba tulimwomba Mungu
Dua angesikia.
2. Una dhiki na maonjo?
Una mashaka pia.
Haifai kufa moyo,
Dua atasikia
Hakuna mwingine mwema
Wa kutuhurumia;
Atujua tu dhaifu;
Maombi asikia.
3. Je, hunayo hata nguvu,
Huwezi kuendelea,
Ujapodharauliwa
Ujaporushwa pia,
Watu wange kudharau,
Wapendao dunia,
Hukwambata mikononi,
Dua atasikia.
Comments
Post a Comment