36. Anisikiaye aliye yote
1. Anisikiaye, aliye yote;
Sasa litangae, wajue wote,
Duniani kote neno wapate,
Atakaye na aje!
Ni “Atakaye”, ni “atakaye”,
Pwani hata bara, na litangae;
Ni Baba Mpenzi alinganaye
Atakaye na aje.
2. Anijiliaye, Yesu asema,
Asikawe, aje hima mapema;
Ndimi njia, kweli, ndimi uzima;
Atakaye na aje!
3. Atakaye aje, ndivyo ahadi;
Atakaye hiyo, haitarudi!
Atakaye lake, ni la abadi!
Atakaye na aje.
Comments
Post a Comment