33. Dhambi ikikulemea
1. Dhambi ikikulemea,
Kwa Bwana rehema;
Hivi sasa tegemea
Neno la salama.
Tegemea, tegemea,
akwita sasa.
Ni Mwokozi, ni
Mwokozi; amini sasa.
2. Yesu amemwaga damu
Ya nyingi baraka;
Nawe sasa oga mumu
Zioshwamo taka.
3. Ni njia yeye hakika
Hwongoza rahani;
Usikawe kumshika,
Uwe barakani.
4. Karibu nawe wingie
Mwetu safarini,
Twende tukamwamkie,
Milele Mbinguni.
Comments
Post a Comment