31. Msingi iMara


1. Msingi imara, enyi wa kweli,
Umekwisha pigwa kwa neno hili;
Aongeze lipi? Mnayo pia
Kwa Yesu mliomkimbilia.

2. Wambiwapo vuka maji ya giza,
Mito ya mashaka taipunguza;
Takupa nawe, nikuwezeshe,
Ipata kufaa, isikutishe!

3. Utakapopishwa ndani ya moto
Nnguvu nitakupa, upate pato;
Huteketezwi, ila taka zako,
Na zitasalia dhahabu zako.

4. Hata zije mvi, walio wangu
Hawaoni kwisha mapenzi yangu;
Nazo zitakapowenea, ndipo
Mabegani mwangu niwatwekapo.

5. Na mtu aliyenitegemea
Kamwe kwa adui sitamtia;
Nguvu za jehanam zijapotisha,
Mtu wangu kamwe sitamuacha.

Comments

Popular posts from this blog

2. Twamsifu Mungu

6. Baba Mwana Roho

7. Ni Tabibu Wa Karibu