30. Nilikuwa kondoo Aliyepotea


1. Nilikuwa kondoo aliyepotea,
Sikupenda zizi kamwe, ila kutembea
Nilikuwa mwana asiyesikia,
Sikupenda baba yangu wala kutulia.

2. Na mchunga mwema alinitafuta,
Baba kwa mapenzi ndiye aliyenivuta;
Karibu ya kufa, kwa kiu na kwa njaa,
Waliniona mnyonge, waliniokoa.

3. Yesu ni mchunga, mwenziwe hapana,
Aliosha taka zangu, dhambi nyingi sana;
Kwa vidonda vyangu alitia dawa.
Ndiye aliyenipata, na kwake nalindwa.

4. Nilikuwa kondoo aliyepotea
Sasa nampenda Baba, na mchunga pia;
Kwanza nilitanga na kukosa sana,
Hivi nyumbani mwa Baba sipotei tena.

Comments

Popular posts from this blog

2. Twamsifu Mungu

6. Baba Mwana Roho

7. Ni Tabibu Wa Karibu