29. Baba yetu aliye Mbinguni


1. Baba yetu aliye Mbinguni
Amenifurahisha yakini
Kuniambia mwake chuoni
Ya kuwa nami Yesu pendoni.

 Anipenda Mwokozi Yesu,
 Anipenda, anipenda;
 Anipenda Mwokozi  Yesu,
 Anipenda mimi.
          
2. Nimuachapo kutanga mbali,
Yeye yu vivyo, hupenda kweli,
Hunirejeza kwake moyoni;
Kweli yu nami Yesu pendoni.

3. Anipenda! Nami nampenda;
Kwa wokovu alionitenda;
Akanifia Msalabani
Kwa kuwa nami Yesu pendoni.

4. Haya kujua yanipa raha;
Kumuamini kuna furaha;
Humfukuza mara shetani,
Kwona yu nami Yesu Pendoni.

5. Sifa ni nyingi asifiwazo,
Moja ni sana katika hizo,
Wala siachi, hata Mbinguni,
Kwimba, “Yu nami Yesu pendoni”.
        

Comments

Popular posts from this blog

2. Twamsifu Mungu

6. Baba Mwana Roho

7. Ni Tabibu Wa Karibu