28. Anipenda Kweli
1. Anipenda ni kweli;
Mungu anena hili;
Sisi wake watoto;
kutulinda si zito.
Yesu anipenda,
Yesu anipenda,
Kweli anipenda,
Mungu amesema.
2. Kwa kupenda akafa
Niokoke na kufa;
Atazidi taka,
Sana ataniweka.
3. Anipenda kabisa;
Niuguapo sasa
Anitunza Mbinguni
Nniliyelala chini.
4. Kunipenda haachi,
Tu sote hapa chini
Baada ya mashaka
Kwake tanipeleka.
Comments
Post a Comment