25. Nimekombolewa na Yesu
1. Nimekombolewa na Yesu
Aliyenirehemia;
Kwa bei ya mauti yake
Nimekuwa mtoto wake.
Kombolewa!
Nakombolewa na damu;
Kombolewa!
Mimi mwana wake kweli.
2. Kukombolewa nafurahi,
Kupita lugha kutamka;
Kulionyesha pendo lake,
Nimekuwa mtoto wake.
3. Nitamwona uzuri wake,
Mfalme wangu wa ajabu;
Na sasa najifurahisha,
Katika neema yake.
4. Najua taji imewekwa
Mbinguni tayari kwangu;
Muda kitambo atakuja,
Ili alipo, niwepo.
Comments
Post a Comment