21. Roho Yangu Hima
1. Roho yangu hima, na taa yako
Kaiwashe vyema, hapa si pako;
Nguvu zote pia za duniani
Hazitakudhuru ukiamini.
Yesu yuko mbele, Yesu yu nyuma,
Yesu vivyo kando, walindwa vyema.
2. Adui shetani, na nguvu zake,
Bwana ameshinda, kwa kifo chake;
Wewe nguvu huna, huna kabisa,
Ndiwe mpungufu, mnyonge hasa.
3. Toka na mapema, mbele ya wote,
Omba, bisha sana, maisha yote;
Vita vikaliko, macho ukae,
Jivike silaha, nawe sishindwe.
4. Bwana Yesu ndiye kwako mchunga,
Neno lake Bwana ndilo upanga;
Mbingu zitakwisha, na nchi pia,
Neno lake Bwana laendelea.
Comments
Post a Comment