20. Ninaye Rafiki Naye
1. Ninaye Rafiki naye
Alinipenda mbele;
Kwa kamba za pendo zake
Nimefungwa milele;
Aukaza moyo wangu,
Uache mageule,
Mimi wake, yeye wangu;
Ndimi naye milele.
2. Ninaye rafiki ndiye
Aliyenifilia;
Alimwaga damu yake
Kwa watu wote pia;
Sina kitu mimi tena,
Nikiwa navyo tele;
Pia vyote ni amana
Ndimi wake milele.
3. Ninaye rafiki naye
Uwezo amepewa;
Atanilinda mwenyewe,
Juu tachukuliwa;
Nikitazama Mbinguni,
Hupata nguvu tele;
Sasa natumika chini,
Kisha juu milele.
4. Ninaye rafiki naye,
Anao moyo mwema;
Ni mwalimu, kiongozi,
Mlinzi wa daima;
Ni nani wa kunitenga
Na mapenzi ya mbele?
Kwake nimetia nanga,
Ndimi wake milele.
Comments
Post a Comment