19. Ndiyo Dhamana Yesu Wangu


1. Ndiyo dhamana, Yesu wangu;
Hunipa furaha za Mbingu;
Mrithi wa wokovu wake
Nimezawa kwa Roho yake.

 Habari njema, raha yangu
 Yesu ndiye Mwokozi wangu,
 Habari njema, raha yangu
 Yesu ndiye mwokozi wangu.

2. Kumsalimu moyo wangu,
Mara namwona raha yangu;
Aniletea malaika,
Wananilinda, taokoka.

3. Sina Kinyume, nashukuru,
Mchana kutwa huja kwangu;
Usiku kucha kuna nuru;
Mwokozi wangu; ndimi huru.

4. Hali na mali anitwaa!
Mara namwona anifaa,
Nami nangoja kwa subira;
Akiniita, nije mara.

Comments

Popular posts from this blog

2. Twamsifu Mungu

17. Namwandama Daima

4. Jina La Yesu Salamu