16. Kumtegemea Mwokozi
1. Kumtegemea Mwokozi,
Kwangu tamu kabisa;
Kukubali neno lake
Nina raha moyoni.
Yesu,Yesu namwamini,
Nimemwona thabiti;
Yesu,Yesu,yu thamani,
Ahadi zake kweli.
2. Kumtegemea Mwokozi,
Kwangu tamu kabisa,
Kuamini damu yake
Nimeoshwa kamili.
3. Kumtegemea Mwokozi,
Kwangu tamu kabisa,
Kwake daima napata
Uzima na amani.
4. Nafurahi kwa sababu
Nimekutegemea;
Yesu,Mpendwa na Rafiki
Uwe nami dawamu.
Comments
Post a Comment