11. Nina Haja Nawe
1. Nina haja nawe
Kila saa;
Hawezi mwingine
Kunifaa.
Yesu, nakuhitaji
Vivyo kila saa!
Niwezeshe, Mwokozi,
Nakujia.
2. Nina haja nawe;
Kaa nami,
Na maonjo haya,
Hayaumi.
3. Nina haja nawe;
Kila hali,
Maisha ni bure,
Uli mbali.
4. Nina haja nawe,
Nifundishe
Na ahadi zako
Zifikishe.
5. Nina haja nawe,
Mweza yote,
Ni wako kabisa
Siku zote.
Comments
Post a Comment